Thursday, April 5, 2012

Tattoo Recordz introducing Triple Divaz

Logo namba moja ya Triple Divaz. 

Logo namba mbili ya Triple Divaz.

Hili ni kundi jipya la muziki la kinadada watatu akiwemo Cianna Jordan, Fantasia na hellens wakiwa chini ya Tattoo Recordz na Richard Manyota kama mratibu mkuu wa kundi hili, "kikubwa watu wanataka mabadiliko katika game n here we are" Mwanadada Fantasia akizungumza kwa niaba ya wenzie, Hellens akajazia "kikubwa watu wasitegemee kutuona tofauti ila wategemee kuona tofauti", Cianna Jordan kwa msisitizo "Hakuna kundi linalojumuisha wadada tupu Tanzania hivyo tunataka kulipa kipaumbele hilo na kuwakilisha mziki mzuri kama wafanyavyo Blue3 kutoka Uganda".

Wakinadada wana confidence ya kutosha juu ya wanachokifanya, nafasi ni yao na ni kweli tunahitaji kuona tofauti, wakizungumzia kuhusu Album ama nyimbo zao kuanza kusikika redio wanashuka "Album hapana kwa kweli bado sana, ila nyimbo soon enough tutaanza kuachia ila kikubwa kwa sasa tunaconcetrate katika project yetu tunayoifanya studio tofauti tofauti ikiwemo Akili Recordz, Tattoo Recordz, Kiumbe, Rama Recordz na nyinginezo nyingi chini ya watayarishaji Akili the brain, Pallah, Elter, Eagle master, Kitah, Jobiso, Ak Musicz na wengineo wengi".

Wednesday, July 27, 2011

A.T na Baby J wamaliza tofauti zao rasmi

A.T katika pozi

Baby J.
Wasanii kioo kunako game ya Bongo wanaotokea visiwani Zanzibar, Baby J na A.T a.k.a Baba ntilie wamemaliza tofauti zao rasmi na kuamua kuachana na mambo ya mabifu wakidai hayana msingi kwani wanachoangalia sasa ni kusonga mbele na kutengeneza pesa, Credit nyingi zinaweza kumuendea mtu mzima G-Lover kwani ndiye aliyekuwa kiungo mchezeshaji kuhakikisha vijana hawa wanarudi upya katika maendeleo,kikao cha dharula kilichofanyika jumanne tarehe 26 mwezi huu wa saba katika sehemu ya vinywaji baridi na chakula ijulikanayo kama MAISHA PLUS ndicho kilichozaa matunda, kikiwahusisha pia watu kadhaa wa karibu na wasanii hao akiwemo mtu mzima SHARO MILIONEA, ALI MASTER, AUNTI kama wenyewe wanavyopenda kumuita ambaye ndiye mmiliki wa mgahawa huo wa Maisha plus, na swala likawa inakuwaje kuhusu nyimbo ambayo Baby J aliitoa akimponda mchizi na baby alikuwa na haya ya kushuka "yale yameshakwisha na A.T ni ndugu yangu hivyo ntaizuia ile nyimbo isipigwe na hata ule mpango wa video hauko tena na nimekubali yaliyopita yamepita" na A.T alikuwa na haya ya kusema "kwa mapatano haya basi tushasameheana na mimi namchukulia Baby J kama mdogo wangu hivyo yameisha na kuonyesha hatuna kinyongo tutagonga ngoma ya pamoja ila kibiashara zaidi", wakati huo huo inasemekana kuna watu hawakufurahishwa na kupatana kwa wasanii hawa kwani walikuwa wanachochea bifu hiyo kwa maslahi yao na wasanii hawa wanapenda watu wafahamu kuwa hawakulazimishwa kupatana ila wamepatana kwani ndicho kitu bora kwao kwa sasa kuliko malumbano yasiyokuwa na msingi, na mwisho kwa pamoja wakashuka "tunajua waliokuwa wanatugombanisha ni watu wetu wa karibu na walikuwa wanafanya hivyo kwa sababu zao na tunashukuru Mungu tumepatana na tumewajua wanafki", Credit zangu za dhati kabisa ziwaendee wasanii hawa kwa kuweka tofauti zao na kuanza maisha upya, lakini pili zimuendee mtu mzima G-lover, Sharo milionea, Ali Master na Aunti wa Maisha plus zanzibar kwa juhudi zao za kiubinadamu kuwaunganisha dada na kaka hawa waliopotea kwa malumbano, HONGERENI SANA BABY J na A.T kwa hatua mlizochukua.
From Tattoo Recordz Management.

A.T na Baby J wamaliza tofauti zao rasmi

A.T katika pozi


Wasanii kioo kunako game ya Bongo wanaotokea visiwani Zanzibar, Baby J na A.T a.k.a Baba ntilie wamemaliza tofauti zao rasmi na kuamua kuachana na mambo ya mabifu wakidai hayana msingi kwani wanachoangalia sasa ni kusonga mbele na kutengeneza pesa, Credit nyingi zinaweza kumuendea mtu mzima G-Lover kwani ndiye aliyekuwa kiungo mchezeshaji kuhakikisha vijana hawa wanarudi upya katika maendeleo,kikao cha dharula kilichofanyika jumanne tarehe 26 mwezi huu wa saba katika sehemu ya vinywaji baridi na chakula ijulikanayo kama MAISHA PLUS ndicho kilichozaa matunda, kikiwahusisha pia watu kadhaa wa karibu na wasanii hao akiwemo mtu mzima SHARO MILIONEA, ALI MASTER, AUNTI kama wenyewe wanavyopenda kumuita ambaye ndiye mmiliki wa mgahawa huo wa Maisha plus, na swala likawa inakuwaje kuhusu nyimbo ambayo Baby J aliitoa akimponda mchizi na baby alikuwa na haya ya kushuka "yale yameshakwisha na A.T ni ndugu yangu hivyo ntaizuia ile nyimbo isipigwe na hata ule mpango wa video hauko tena na nimekubali yaliyopita yamepita" na A.T alikuwa na haya ya kusema "kwa mapatano haya basi tushasameheana na mimi namchukulia Baby J kama mdogo wangu hivyo yameisha na kuonyesha hatuna kinyongo tutagonga ngoma ya pamoja ila kibiashara zaidi", wakati huo huo inasemekana kuna watu hawakufurahishwa na kupatana kwa wasanii hawa kwani walikuwa wanachochea bifu hiyo kwa maslahi yao na wasanii hawa wanapenda watu wafahamu kuwa hawakulazimishwa kupatana ila wamepatana kwani ndicho kitu bora kwao kwa sasa kuliko malumbano yasiyokuwa na msingi, na mwisho kwa pamoja wakashuka "tunajua waliokuwa wanatugombanisha ni watu wetu wa karibu na walikuwa wanafanya hivyo kwa sababu zao na tunashukuru Mungu tumepatana na tumewajua wanafki", Credit zangu za dhati kabisa ziwaendee wasanii hawa kwa kuweka tofauti zao na kuanza maisha upya, lakini pili zimuendee mtu mzima G-lover, Sharo milionea, Ali Master na Aunti wa Maisha plus zanzibar kwa juhudi zao za kiubinadamu kuwaunganisha dada na kaka hawa waliopotea kwa malumbano, HONGERENI SANA BABY J na A.T kwa hatua mlizochukua.
From Tattoo Recordz Management.

Monday, July 18, 2011

Tattoo Recordz Kuwatoa Wasanii Wapya Wa Shindano la Jenga Nchi Yako

Mkurugenzi na mmiliki wa Tattoo Recordz akiwa ofisini kwake Masaki,DSM

Hapa ni nje ya Studio za Tattoo Recordz
Mkurugenzi wa Tattoo Recordz akiwa na meneja wa studio Abi MP

Hivi karibuni kuna mchakato wa kuchukua fomu ambao unaendelea kuhusu tamasha la kusaka vipaji linaliokwenda kwa jina la jenga nchi yako,likiwa limetayarishwa na Richard Manyota kama mratibu kutoka kampuni ya global publishers ambao ni watengenezaji wa magazeti ya ijumaa,uwazi,risasi,amani na champion,kwa kushirikiana na Police tanzania ambao ni wadhamini wakuu,lengo ni kupunguza lindi la uhalifu na kufanya Tanzania salama kupitia vipaji vijana walivyonavyo, na kama sehemu ya kuunga mkono harakati zote za kuleta amani na ajira kwa vijana Tattoo Recordz kupitia Mkurugenzi wake mkuu Bw Faraja kiobya Leguna ama Brother Tattoo kama anavyofahamika imetoa nafasi ya kurekodi kwa washindi watakaopatikana katika shindano hilo,brother Tattoo anashuka "sioni sababu ya kutowasaidia wasanii wachanga kutimiza ndoto zao kwani hata mimi mwanzo nilikuwa msanii na nafahamu ni adha gani wasanii wachanga wanazopata" ,shindano hilo litashirikisha wasanii ambao hawakuwahi kurekodi ama kuskika redioni tu, na fomu bado zinapatikana katika ofisi za global publishers bamaga na kwa maelezo zaidi soma magazeti pendwa yanayotengenezwa na global publishers niliyoyaorodhesha hapo juu.

Friday, July 15, 2011

24 Bars za Mexican ni zaidi ya pigo kwa Bagdadi - X.Dizzo




X-Dizzo on the pose

X-Dizzo with Brother Tattoo

X on tha P

X ma nicca riddin it

X with Wakweli and Mwajo
Jamaa anaitwa X-dizzo na Temeke ndio wilaya anayotokea, mchizi akiwa na hasira za kutosha anazungumzia swala juu ya kipande cha mistari kinachoitwa 24 bars za mexicana, X anashuka "unajua Bagdadi alikuwa mwanangu kichizi lakini mchizi bonge la snitch, tunafanya harakati wote tukijua mwana wa ukweli kumbe nyoka na mwisho wa siku anafanya ngoma anatuponda machizi wake wa harakati, amesahau kuwa na yeye alikuwa huko huko", so X ndo anashuka kimtindo huo kimaneno na kwenye ngoma mchizi anaanza na ryrics zinazosema "Hakuna Mexi bila cana wasichana lacavela bila puti nawafunga nawafanya mpaka jela", mchizi anazidi kushuka "nawajua mnanijua siogopi kufanya, mkizingua nazingua siogopi kuhanya", mchizi anazidi "Bagdadi umekutana na mmarekani, kwenye stanza nakutupa nakuficha kwapani", hayo si maneno yangu ni maneno ya mtu mzima X-Dizzo katika kipande cha 24bars za mexicana, na kipande hicho kinapatikana katika playlist ya Tattoo Recordz kwa download na kusikiliza.

Monday, July 11, 2011

Je unajua kilichomkuta mnyama juzi

mnyama wakati akijipigia debe siku moja kabla

Ha ha ha ha hichi ndicho kilichomkuta,kumbe demu mke wa mtu alafu mumewe mmasai.

siku ya jumapili ndani ya viwanja vya jangwani ilikuwa ni shamra shamra,nderemo na vifijo baada ya mnyama kuchinjwa hadharani ndani ya uwanja mpya wa taifa jijini Dar es saalam, goli moja tu la kichwa kipindi cha pili za dakika za nyongeza lililotiwa kimiani na njema ya miraba minne kama sio sita na kuipa yanga african sports club ubingwa wao wa mara ya pili wa kombe la CECAFA, haya simba aliomba kupewa,yanga akamhakikishia yeye tu na spidi yake na matokeo yake simba kapakatwa pub,Hongera yanga FC.

Monday, June 13, 2011

Grand new Tattoo Recordz Yakamilika Pande za Masaki

Mamparado akipaka rangi

Mkurugenzi akiwa kazini kuwaonyesha vijana wake kazi inavyofanywa

Meneja nae hakuwa nyuma,si unajua anapenda sana mayai basi yeye na trey tu. 
Mkurugenzi wa Tattoo akipaka rangi,mmmh jamaa kweli noma hadi kupaka rangi anajua

hapa akiwaelekeza jambo vijana wake

Da hii kazi kweli itaisha mbona ndo kama inaanza

hatimaye inaanza kukamilika,na hiyo ndiyo ofisi ya mkurugenzi hapo hapo studio masaki

hapa mkurugenzi akiwa na azma kutoka UMABE

hapa ni nje ya mjengo iliko Tattoo Recordz

dizaini kama lazima upande ghorofa hivi ndo uingie Tattoo Recordz,hapa mkurugenzi na meneja Abi

Walisema hayawi hayawi, hatimaye New Tattoo Recordz inaanza mzigo na producer AK MUSICZ akiwa mtamboni.
Hizo zote ni harakati na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Tattoo Recordz kusimama Masaki,so wadau, wapenzi, wasanii na mashabiki, Tattoo Recordz imehamia rasmi Masaki Chore Road karibu na slipway, mawasiliano yaleyale na kazi zile zile ,ONE LOVE.

Tuesday, May 17, 2011

Abuu Zaidi - Mwanzo Mwisho Ni Zaidi Ya Abuu Kutoka Tattoo Recordz

Abuu Zaidi

Abuu Zaidi katika pozi

Abuu Zaidi katika pozi na dogo wake
Michoro ya Hiphop toka British Council


Abuu Zaidi na wanafunzi wenzake

Jamaa akiwa ni kipaji kipya kutoka pande za mwenge anayepiga mzigo katika studio ya Tattoo Recordz na memba mpya wa kundi lililowahi kutikisa wakati muziki wa Hiphop ndo unaanza Bongo yaani K.Crew, akiwa anasimamiwa vilivyo na mwanaharakati wa Hiphop Zavara ama Chief Ramso huyu ni Abuu Zaidi toka mwenge,ni mmoja kati ya wanahiphop waliopata kuonyesha vipaji vyao katika harakati za Hiphop zilizokuwa zinafanyika British Council chini ya mtu mzima Zavara,na sasa akiwa chini ya Tattoo Recordz ameshafanya ngoma kibao na zinasubiri muda tu,ngoma hizo zimefanyika chini ya watayarishaji Pallah na AK47 ama Bunduki wote kutoka Tattoo Recordz,na kinachofanya tumzungumzie leo ni ngoma yake mpya na ya kwanza kuachiwa inayoitwa MWANZO MWISHO ikiwa ni mkono wa AK47,yeye mwenyewe anasema "hii ngoma yangu ya mwanzo mwisho ni zaidi ya mimi,nataka watu wajue kuwa kuna watu waliobaki kwenye Hiphop si hao tu wanaoskika pekee", Abuu Zaidi ndio jina, Mwanzo mwisho ndio ngoma,yuko mtaani na ngoma hii itapatikana katika playlist yetu katika blog hii soon,get ready 4 Abuu Zaidi.

Friday, May 6, 2011

Wajue Wana Hiphop Wanaoongoza Kwa Kuingiza Mkwanja Mkubwa Kwa Mwaka.

Wakati wana Hiphop na wanamuziki wa Tanzania wakiwa katika vita dhidi ya wezi na wanyonyaji wa kazi zao,duniani kote haswa nchini marekani vita hiyo imeonekana ni jambo lililosahaulika kabisa na watu wanazungumzia nani ana mzidi mwenzake kwa pesa na nani ana miliki nini,wakati pato la mwanamuziki wa marekani likifikia takribani dola milioni sitini kwa mwaka nchini tanzania shilingi milioni sitini tu za kibongo bado ni ndoto kuwa ni mapato ya mwanahiphop kwa mwaka,si kuwa haipatikani la hasha,wizi,ukilitimba,zulma na kutojua haki zetu za msingi ndiko kunafanya tusiwe na kipato chochote cha kueleweka kwa mwaka.

Na Hii ndiyo List ya wanahiphop wanaoongoza kwa mkwanja mrefu nchini Marekani. 
Jamaa anawaongoza wenzake kwa mwaka wa pili sasa anaitwa Shawn Carter a.k.a Jay Z akiwa anatokea Lebo ya Rocca Fella, akiwa hewani na ngoma kama Empire state of mind, Run this town na own to the next one, amefanikiwa kuingiza kiasi cha Dolla milioni 65 kwa mwaka uliopita na kumfanya kuwa msanii wa Hiphop aliyeingiza mkwanja wa maana kwa mwaka uliopita na kuwaburuza wakongwe na mastaa kibao.

Sean Combs P.diddy ndo jina,akiwa anatokea Lebo ya Bad Boys jamaa amefanikiwa kuingiza kiasi cha Dolla milioni 30 kwa mwaka ikiwa ni nusu ya kipato alichoingiza Jay Z,Diddy anakumbukwa kwa vibao vyake matata kama I Need A Gal part 1&2 ,jamaa ameingiza mkwanja huo kutokana na show za muziki,matangazo,mauzo ya album na biashara zake.

Jina kamili Alluane Thaim a.k.a Akon akiwa na asili ya nchini senegal,jamaa ni bosi wa Lebo ya Convict Music na msanii ambaye ametokea kuiteka jamii ya Hiphop kwa miaka sasa,watu wanaweza kujiuliza jamaa anawezaje kuwa katika kundi la Hiphop yet anaimba,kiukweli jamaa anapatikana humu kutokana na ushiriki wake katika mziki mzima wa hiphop,katika kipindi cha mwaka mmoja jamaa amefanikiwa kuingiza kiasi cha Dolla milioni 21 na kumfanya kuwa namba tatu kwa wanahiphop walioingiza mkwanja wa kutosha.

Weezy Weezy ndivyo anavyopenda aitwe,jina la kitambulisho Dwayne Carter a.k.a Lil Wayne kutoka Lebo ya Cash Money,akiwa na ngoma kama Fire Man,Prom Queen,Lolipop,Mr Carter jamaa ndiye anayekamata namba nne kwa kufanikiwa kuingiza kiasi cha Dolla milioni 20 kwa mwaka.

Andre Young a.k.a Dr Dre akiwa ni msanii mkongwe na producer wa siku nyingi pia,akiwa na historia ya kutoa wasanii wanaokamata kwa muda mrefu katika gemu na wengi wanakumbuka kuwa ndiye producer aliyekuwa anatengeneza ngoma za 2pac,baadae Eminem,50cent,Mob Deep,snoop na wengineo wengi,Lebo inaitwa Interscope na jamaa amefanikiwa kuingiza kipato cha dolla milioni 17 kwa mwaka na kushika namba tano. 

Ludacris ndilo jina la kipato,Christopher Bridges ndilo jina la kitambulisho jamaa akiwa na ngoma kama Move,Money maker,stand up na album kadhaa mkononi kwa mwaka uliopita alifanikiwa kuingiza kiasi cha Dolla za kimarekani milioni 16 na kushika namba 6.

Calvin Broadus a.k.a Snoop Dogg a.k.a The Pimp akiwa na album mpya inayokwenda kwa jina la Doggumentally anashika nafasi ya saba kwa kuingiza kiasi cha Dolla milioni 16 kwa mwaka uliopita kupitia muziki,filamu na biashara.

Timberland a.k.a Timothy Mosley akiwa producer na msanii wa muda mrefu,anashika namba nane kwa kuingiza kiasi cha Dolla milioni 14 kwa mwaka uliopita.

Pharrel Williams ndio jina,jamaa hana a.k.a na amepata umaarufu kupitia kundi la NERD,jamaa kwa mwaka uliopita alifanikiwa kuingiza kiasi cha Dolla milioni 13.

Kanye West akiwa ni producer na pia ni msanii mkongwe wa Hiphop kwa mwaka uliopita alifanikiwa kuingiza kiasi cha Dolla milioni 12 na kumfanya kushika namba kumi katika wasanii wa hiphop walioongoza kwa kuingiza pato kubwa kwa mwaka.

Wakati wengine wakijivunia muziki kama sehemu ya eneo la kuingiza kipato bado Tanzania inachukulia muziki kama sehemu ya burudani tu, INASIKITISHA. 

Thursday, May 5, 2011

Osama Bin Laden Na Kifo Cha Bei Rahisi Kinachowafanya Wengi Wasiamini.

Osama Bin Laden

Obama akitangaza kifo cha Osama

Wananchi wakishangilia Ground Zero

Tangazo la kutafutwa kwa Osama

Osama katika gwanda za jeshi

Picha Feki ya kifo cha Osama

Eneo la tukio linalodaiwa Osama alikouliwa

kipeperushi kutoka serikali ya marekani kikielezea juu ya kutafutwa kwa Osama

Jumapili tarehe 02/05/2011 Dunia ilipatwa na mshangao pale Rais wa Marekani bwana Barrack Obama aliposimama na kuutangazia Umma na Dunia juu ya kumuua Osama Bin Laden, kiongozi wa kundi la Al Qaeda ambaye kwa miaka takriban kumi sasa alikuwa akitafutwa na marekani kwa udi na uvumba,lakini taarifa hiyo ikiwaacha watu wengi na mshangao na maswali kwa kuwa na mapungufu mengi na yanayoonekana kutokuwa na uhalisia juu ya kifo cha Jemedari huyo wa kundi la Al Qaeda aliyepata kuisumbua marekani na kuipa historia ya tukio la 9/11 na kumuongezea umaarufu zaidi ya ule aliokuwa nao mwanzo,taarifa hiyo ilipotoka si wote walioikubali na kuna sababu nyingi iliyofanya iwe hivyo.

HIZI NDIZO SABABU KUMI NA MOJA (11) ZINAZONIFANYA MIMI BINAFSI KUUNGANA NA MAMILIONI YA WATU DUNIANI KOTE WASIOAMINI JUU YA KIFO HICHO.
(1).Wapakistani kukikataa kifo hicho,Marekani ikiwa inadai Pakistani ndiko mauaji ya Osama yalikofanyika Raia wengi wa nchi hiyo wamekataa kukikubali kifo hicho kwa jinsi mazingira ya kifo yalivyoandaliwa kwani inaonyesha wazi toka mwanzo haikuwa rahisi kwa Osama kuishi nchini humo, na hata Raisi wa Pakistani alishawahi kukanusha juu ya kujificha Osama nchini kwake akieleza kuwa kwa jinsi Pakistani inavyoishi sio rahisi kwa mtu kuishi bila kufahamika na watu wengine,kwani watu wa Pakistani wanaishi kwa kufahamiana pengine kuliko hata nchi nyingine yoyote duniani.
(2).Picha ya Uongo ya kifo cha Osama,watu wengi wakiwa wanaanza kuikubali taarifa ya kifo hicho kulikuja kuzuka habari kuwa picha zilizotolewa sio za kweli kwani mazingira ya kifo,nguo zinazoonekana katika picha,sehemu ya bega na uso havikuendana hivyo hakukuwa na uhalisia wowote wa kuunganisha picha hiyo na mazingira yanayoizunguka,na baadae U.S officials walikuja kutoka tamko la kuonya kuwa picha hiyo ni feki kwa kituo cha NBC news,sasa swali ni je picha halali ya Osama akiwa amekufa ziko wapi?.
(3).Sehemu aliyozikiwa baada ya kufa,hili ni jamo lingine lililoishangaza dunia,wakati marekani inadai imeutupa ama kuuzika mwili huo baharini dunia ya werevu imekataa na mimi nikiwamo kwani tunakumbuka jinsi wamarekani walivyokuwa wakimsaka Osama na hata Kuandika wanamtaka akiwa DEAD or ALIVE hivyo hawawezi kutuambia mtu huyu waliyetumia mabilioni ya dola kumsaka baada ya kumuua wakamtupa kirahisi baharini bila kuuonyesha ulimwengu nini walichomfanya ili iwe fundisho kwa watu wa aina yake,NO hiyo haingii akilini hata chembe,na kufanya jambo liwe gumu vyombo vya habari ikiwemo Al Jazeera vimefatilia kwa karibu juu ya swala la maziko hayo na kusema bado ni utata huku akilini mwa watu wengi jibu likiwa ni UONGO MTUPU kama sio WIZI MTUPU.
(4).Kutopatikana hata tukio moja wakati wanajeshi wakivamia na kushambulia eneo alilodaiwa kuuawa Osama,Wakati Dunia inafahamu nguvu ya teknolojia ya taifa la marekani na kumekuwa na mazoea aidha ya kupata picha za moja kwa moja (live feed) ama marudio ya tukio baada ya kutokea wakati marekani ikiwanyaka maadui zake, tumeona hiyo kwa Sadam Hussein wakati anakamaywa,na magaidi kadhaa waliopatwa kukamatwa hivyo huwezi kutuambia tukio la kumkamata na kumuua gaidi huyo aliyeifanya marekani ikaingia katika kitabu cha kumbukumbu ya tukio la september eleven haikuwa muhimu kiasi hicho kuonekana duniani kwa faida ya wamarekani na dunia nzima,ina maana hakukuwa na camera au satelite eneo la tukio,au hawakupenda kumdhalilisha kama walivyomdhalilisha Sadam Husein kwa kumnyonga hadharani dunia ikishuudia Live?,kwangu hiyo nayo ni propaganda kama zilivyo fact tatu zilizotangulia,hivyo marekani bado ina kazi ya kutuelewesha zaidi.
(5).Kufa kirahisi kwa kupigwa risasi kichwani,kila mtu anafahamu what Osama Bin Laden is capable of,hivyo marekani itupe sababu ama picha kamili ya kilichotokea mpaka jamaa huyu akapigwa risasi kichwani kirahisi kiasi hicho,swali ni je kama alikamatwa kisha kupigwa risasi kwa nini hawakumsafirisha mtu huyu marekani kwani alikuwa akitakiwa DEAD or ALIVE,na kwa kuwa ni jambo la ulimwengu mzima sasa kwa nini wasitueleze jinsi tukio zima lilivyotokea,labda ni mwanajeshi yupi anahusika na kifo cha gaidi huyo ili dunia impongeze na kumpa haki yake ya ushujaa,zaidi ya kutuambia tumemuua kwa risasi ya kichwa.
(6).Eneo la tukio alilodaiwa kuuawa Osama,katika picha zinazoonyeshwa na vyombo vya habari ni picha tu ya chumba kikiwa na kitanda,nguo kadhaa na damu ikiwa imezagaa,swali ni je kuna chochote kinachothibitisha hilo ni eneo la tukio ya kifo hicho,au ni nyumba tu kama nyumba nyingine yoyote inayoweza kuwepo katika eneo lolote duniani ikiwa na kitanda,nguo na damu?,na kama tukio la kukamatwa na kuuawa lipo katika video basi lingetuonyeshwa nyumba ama chumba hicho na kutufanya tuamini kweli ni sehemu husika.
(7).Obama kukataa kutoa picha za mwili wa Osama,wakati dunia ikitafakari juu ya ukweli halisi mshangao mwingine unakuja wakati rais Obama anapokataa kutoa picha za marehemu Osama Bin Laden,aliyazungumza hayo akiongea na mwandishi Steve Kroft wa kituo cha CBS news,kisingizio ni kuwa picha hizo hazifai kuonekana hadharani,sasa swali ni je kati ya kumnyonga mtu hadharani dunia ikishuhudia na kutoa picha ya maiti iliyouawa kipi ambacho hakifai kuonekana hadharani?,tumeona jinsi gani marekani inavyoweza kuwadhalilisha adui zake sasa iweje iwe na aibu na huyu aliyeuwa maelfu ya wamarekani, wakati ilimnyonga Sadam ambaye hakuuwa hata raia mmoja wa kimarekani na hakuwa akitafutwa tuliona tukio zima licha ya haki za binadamu kupiga kelele.
(8).Ukimya wa Osama kwa miaka mingi sasa,Kuna watu wanalazimika kuamini kuwa marekani hawakumuua Osama na hajafa,na kama amekufa basi si wao wamarekani waliomuua,Osama amekuwa kimya kwa miaka mingi sasa na hata baadhi ya vyombo vya habari kuamini alishakufa,hakuonekana,kuzungumza wala kuonyesha dalili zozote za uwepo wake duniani,hivyo kuna asilimia kubwa kuwa kama ni kufa basi alikufa kwa matatizo ama maradhi mengine na si wamarekani na ndio sababu wamarekani hawana picha,video hata sauti ya tukio la mauaji yake na hawawezi kuthibitisha kifo hicho kwa vitendo.
(9).Kuuawa kirahisi baada ya kuwasumbua miaka zaidi ya kumi,tunafahamu kuwa Bill Clinton alimtafuta kimya kimya,George Bush akamtafuta kwa kelele na mbwembwe nyingi na hakufanikiwa kukamata hata nguo alizokuwa anavaa Osama,sasa leo iweje Obama ambaye hata hakuonyesha nia ya kushughulika na jamaa huyo kuibuka kidedea tena kirahisi kwa kumpiga risasi kichwani na kumtupa baharini,inaonekana basi Obama hataki makuu kwani kamuua osama kimya kimya pia hakutaka picha zozote za video zichukuliwe,na sasa hataki hata kutuonyesha picha za marehemu kwani Osama hakuwa BIG DEAL KWAKE.
(10).Kifo hicho kuhusishwa na uchaguzi mkuu ujao wa marekani,wote tunakumbuka moja kati ya vitu vilivyompa kura nyingi na kumuingiza madarakani Obama mwaka 2008 ni swala la kutaka kulifunga gereza la Guantanamo bay,na kuwarudisha wanajeshi wa marekani kutoka Iraq na Afganistani,lakini miaka imekatika na uchaguzi wa awamu ya pili umewadia Rais huyo akiwa hajatimiza ahadi zake hizo kwani Guantanamo bay bado iko na mateso yake yakiendelea kama kawaida,na wanajeshi Afganistani wakiendelea na mbilinge zao za vita hiyo ya kila siku isiyoisha,wachunguzi wa mambo wanathubutu kusema kifo hiki cha kupandikizwa ni njia ya kumuongezea umaarufu Obama na kumpa nafasi ya kuchukua tena kiti chake cha urahisi kwani kushindwa kwake kutekeleza ahadi zake zile mbili ilikuwa ni kuti kavu ambalo bila shaka lingemuangusha Obama katika Uchaguzi mkuu mwakani.
(11).Hisia ya marekani kutaka sifa kwa jambo lisilowahusu,swali ni je gaidi yeyote wamarekani wanaomtafuta hawezi kufa kwa uwezo wa mungu mpaka wao wamkamate au kumuua?,inawezekana kweli Osama amekufa lakini si wamarekani waliomuua na inawezekana alishakufa miaka mingi sana na ndo maana alikuwa kimya kwa kipindi kirefu bila kuzungumza chochote,na wamarekani inawezekana wamepata nafasi ya kugundua hilo siku za karibuni na kuamua kulitungia hoja,mwandishi Mark Pasetsky anasisitiza kuwa kuna ulazima wa picha za Osama akiwa amekufa zitolewe ili kumaliza utata wa kifo hicho na kama ni kuipa credit marekani basi tuipe kihalali na si kwa kusubiri mtu ajifie mwenyewe sifa wapate wao.
Huo ni mtazamo wangu na si hoja,pia hauhusiani na upande wowote.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...