Tuesday, May 17, 2011

Abuu Zaidi - Mwanzo Mwisho Ni Zaidi Ya Abuu Kutoka Tattoo Recordz

Abuu Zaidi

Abuu Zaidi katika pozi

Abuu Zaidi katika pozi na dogo wake
Michoro ya Hiphop toka British Council


Abuu Zaidi na wanafunzi wenzake

Jamaa akiwa ni kipaji kipya kutoka pande za mwenge anayepiga mzigo katika studio ya Tattoo Recordz na memba mpya wa kundi lililowahi kutikisa wakati muziki wa Hiphop ndo unaanza Bongo yaani K.Crew, akiwa anasimamiwa vilivyo na mwanaharakati wa Hiphop Zavara ama Chief Ramso huyu ni Abuu Zaidi toka mwenge,ni mmoja kati ya wanahiphop waliopata kuonyesha vipaji vyao katika harakati za Hiphop zilizokuwa zinafanyika British Council chini ya mtu mzima Zavara,na sasa akiwa chini ya Tattoo Recordz ameshafanya ngoma kibao na zinasubiri muda tu,ngoma hizo zimefanyika chini ya watayarishaji Pallah na AK47 ama Bunduki wote kutoka Tattoo Recordz,na kinachofanya tumzungumzie leo ni ngoma yake mpya na ya kwanza kuachiwa inayoitwa MWANZO MWISHO ikiwa ni mkono wa AK47,yeye mwenyewe anasema "hii ngoma yangu ya mwanzo mwisho ni zaidi ya mimi,nataka watu wajue kuwa kuna watu waliobaki kwenye Hiphop si hao tu wanaoskika pekee", Abuu Zaidi ndio jina, Mwanzo mwisho ndio ngoma,yuko mtaani na ngoma hii itapatikana katika playlist yetu katika blog hii soon,get ready 4 Abuu Zaidi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...