Friday, May 6, 2011

Wajue Wana Hiphop Wanaoongoza Kwa Kuingiza Mkwanja Mkubwa Kwa Mwaka.

Wakati wana Hiphop na wanamuziki wa Tanzania wakiwa katika vita dhidi ya wezi na wanyonyaji wa kazi zao,duniani kote haswa nchini marekani vita hiyo imeonekana ni jambo lililosahaulika kabisa na watu wanazungumzia nani ana mzidi mwenzake kwa pesa na nani ana miliki nini,wakati pato la mwanamuziki wa marekani likifikia takribani dola milioni sitini kwa mwaka nchini tanzania shilingi milioni sitini tu za kibongo bado ni ndoto kuwa ni mapato ya mwanahiphop kwa mwaka,si kuwa haipatikani la hasha,wizi,ukilitimba,zulma na kutojua haki zetu za msingi ndiko kunafanya tusiwe na kipato chochote cha kueleweka kwa mwaka.

Na Hii ndiyo List ya wanahiphop wanaoongoza kwa mkwanja mrefu nchini Marekani. 
Jamaa anawaongoza wenzake kwa mwaka wa pili sasa anaitwa Shawn Carter a.k.a Jay Z akiwa anatokea Lebo ya Rocca Fella, akiwa hewani na ngoma kama Empire state of mind, Run this town na own to the next one, amefanikiwa kuingiza kiasi cha Dolla milioni 65 kwa mwaka uliopita na kumfanya kuwa msanii wa Hiphop aliyeingiza mkwanja wa maana kwa mwaka uliopita na kuwaburuza wakongwe na mastaa kibao.

Sean Combs P.diddy ndo jina,akiwa anatokea Lebo ya Bad Boys jamaa amefanikiwa kuingiza kiasi cha Dolla milioni 30 kwa mwaka ikiwa ni nusu ya kipato alichoingiza Jay Z,Diddy anakumbukwa kwa vibao vyake matata kama I Need A Gal part 1&2 ,jamaa ameingiza mkwanja huo kutokana na show za muziki,matangazo,mauzo ya album na biashara zake.

Jina kamili Alluane Thaim a.k.a Akon akiwa na asili ya nchini senegal,jamaa ni bosi wa Lebo ya Convict Music na msanii ambaye ametokea kuiteka jamii ya Hiphop kwa miaka sasa,watu wanaweza kujiuliza jamaa anawezaje kuwa katika kundi la Hiphop yet anaimba,kiukweli jamaa anapatikana humu kutokana na ushiriki wake katika mziki mzima wa hiphop,katika kipindi cha mwaka mmoja jamaa amefanikiwa kuingiza kiasi cha Dolla milioni 21 na kumfanya kuwa namba tatu kwa wanahiphop walioingiza mkwanja wa kutosha.

Weezy Weezy ndivyo anavyopenda aitwe,jina la kitambulisho Dwayne Carter a.k.a Lil Wayne kutoka Lebo ya Cash Money,akiwa na ngoma kama Fire Man,Prom Queen,Lolipop,Mr Carter jamaa ndiye anayekamata namba nne kwa kufanikiwa kuingiza kiasi cha Dolla milioni 20 kwa mwaka.

Andre Young a.k.a Dr Dre akiwa ni msanii mkongwe na producer wa siku nyingi pia,akiwa na historia ya kutoa wasanii wanaokamata kwa muda mrefu katika gemu na wengi wanakumbuka kuwa ndiye producer aliyekuwa anatengeneza ngoma za 2pac,baadae Eminem,50cent,Mob Deep,snoop na wengineo wengi,Lebo inaitwa Interscope na jamaa amefanikiwa kuingiza kipato cha dolla milioni 17 kwa mwaka na kushika namba tano. 

Ludacris ndilo jina la kipato,Christopher Bridges ndilo jina la kitambulisho jamaa akiwa na ngoma kama Move,Money maker,stand up na album kadhaa mkononi kwa mwaka uliopita alifanikiwa kuingiza kiasi cha Dolla za kimarekani milioni 16 na kushika namba 6.

Calvin Broadus a.k.a Snoop Dogg a.k.a The Pimp akiwa na album mpya inayokwenda kwa jina la Doggumentally anashika nafasi ya saba kwa kuingiza kiasi cha Dolla milioni 16 kwa mwaka uliopita kupitia muziki,filamu na biashara.

Timberland a.k.a Timothy Mosley akiwa producer na msanii wa muda mrefu,anashika namba nane kwa kuingiza kiasi cha Dolla milioni 14 kwa mwaka uliopita.

Pharrel Williams ndio jina,jamaa hana a.k.a na amepata umaarufu kupitia kundi la NERD,jamaa kwa mwaka uliopita alifanikiwa kuingiza kiasi cha Dolla milioni 13.

Kanye West akiwa ni producer na pia ni msanii mkongwe wa Hiphop kwa mwaka uliopita alifanikiwa kuingiza kiasi cha Dolla milioni 12 na kumfanya kushika namba kumi katika wasanii wa hiphop walioongoza kwa kuingiza pato kubwa kwa mwaka.

Wakati wengine wakijivunia muziki kama sehemu ya eneo la kuingiza kipato bado Tanzania inachukulia muziki kama sehemu ya burudani tu, INASIKITISHA. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...