Producers.

Idrisa Hashim a.k.a AK47
Jamaa akiwa katika umri mdogo tu ameweza kuonyesha kipaji cha hali ya juu katika kutengeneza midundo ya hiphop,R n B,Reggae,Gospel,Kwaito,bongo fleva,crunk na akiwa ndiye mpishi wa midundo ya nyimbo ya msanii Nash Mc inayoitwa mchawi ndugu,yeye binafsi ana usemi anaopendelea kusema "music is my soul,and i can feel it flowing inside me", then anasema pia "music can change the world because it can change people",huyo ni AK47 si mimi,ila naungana nae moja kwa moja katika semi zake zote mbili.

Athumani Palla a.k.a Pallah (mwenye mavazi meusi)
Mchizi anapiga mzigo Radio uhuru kama mhariri wa habari lakini afta that tunakutana pale kati kunako tattoo recordz,ni mmoja kati ya watayarishaji wachache wenye uwezo wa kuchochoa (choping) beat na kuitumia anavyohitaji yeye,jamaa anagonga Hiphop kwenda mbele,haimaanishi hafanyi mziki wa aina nyingine,la hasha,anagonga pia R n B,Zouk,Bongo fleva,na kazi ya kwanza inamtambulisha kunako game ni nyimbo ya Nash Mc inayoitwa HOMA IMENIZIDIA akiwa amechop midundo ya nyimbo ya zilipendwa ya mzee wetu Bitchuka na kusababisha utata mkubwa ambao baadae uliisha kwa pande zote mbili kukubali matokeo.

Erick a.k.a Elter
Jamaa anaitwa ELTER akiwa anatokea mkoani Arusha Hiphop ilikolala,akiwa ni mmoja kati ya watayarishaji wazuri wa mziki wa Hiphop,jamaa akiwa amefanya ngoma ya msanii Sapeleme inayoitwa Ngada boy(inapatikana kwenye playlist ya music by Tattoo),anafanya mtindo wa R n B,Zouk,Kwaito,Mchiriku lakini akiwa na mapenzi ya ziada kwa Hiphop.

Steve joseph a.k.a Jobiso (Baba Byson)
Wengi watakumbuka jina SMALL JOBISO,yeahmen ila kwa sasa si small tena,bali Jobiso a.k.a Baba Bayson akiwa ni Head of producers from tattoo recordz,jamaa anastahili sifa za kutosha kwa kazi kubwa anayoionyesha,akiwa amefanya kazi ya Buibui inayoitwa BORA NIIMBE (ipo katika Tattoo music playlist),pia akiwa ndiye mtayarishaji aliyemgongea midundo msanii Beka katika nyimbo yake ya NATUMAINI REMIX,lakini pia akifanya kazi ya Maunda inayoitwa NALIA.Big up Baba Bayson.

Kama Watayarishaji mtu anaweza kuuliza kwani ni wao na si watu wengine,kwanza ni vijana,wenye vipaji na mitazamo mipya katika muziki.
,
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...