Record Label

Tattoo recordz Recordz kama studio ina watu wa label wapatao saba,ni vijana wenye vipaji tofauti na wenye moyo wa mziki,wa kwanza ni Cianna Jordan,Valley,Nas Jalala,Evance Mc,Kazo,Sharaipa,Sapeleme lakini pia kuna wasanii tofauti ambao kwa wakati na kila mmoja ana mkataba maalum wa kufanya kazi na Tattoo akiwamo Nash Mc,Emax,Beka,Abi the gutterlist.


Cianna Jordan
Huyu ni first lady wa Tattoo Recordz,akiwa anajiandaa kutoka na song moja matata inayoitwa WEWE NI NANI,ni ngoma inayobamba vilivyo na ina kila aina ya ladha katika mtindo wa zouk.
Cianna Jordan katika pozi
Cianna akiwa na producer wake AK47
Cianna akiwa na mkurugenzi wa Tattoo Recordz Gbroo a.k.a Tattoo


SHARAIPA
Jamaa anapiga bonge moja la R n B na akiwa anasubiri muda wake wa kutoka ufike soon tutakujuza lini na nyimbo gani jamaa ataiachia.
Sharaipa akiwa na meneja wa Tattoo Recordz Abi the Rapper
Sharaipa akiwa kwenye pozi


SAPELEME
Jamaa akiwa anafanya mtindo wa Hiphop na ngoma inayomsogeza karibu kwa wadau inaitwa Ngada Boy na Mtaa wa pili kimenuka,ngada boy inapatikana katika playlist yetu ya front page n mtaa wa pili soon enough itakuwapo pia,jamaa ana uwezo so more love n more support,HIPHOP FOR LIFE.
Msanii Sapeleme akiwa kwenye pozi


VALLEY
Hii ni lulu kama si nyota inayoing'arisha Tattoo Recordz,bwana mdogo ana kwenda kwa jina la Valley toka pande za msasani,na ngoma inayokuja kumtambulisha kwenu inaitwa ZIGO LA MOTO ni bonge moja la R n B n likiachiwa litakuwa kwa playlist yetu.

NAS TYSER
Bwana mdogo akiwa anafanya aina zote za muziki wa bongo fleva,Zouk,Mchiriku,Kwaito mpaka R n B,anaitwa Nas Tyser toka pande za M/Nyamala na anajiandaa andaa wakati wake ukifika soon atakuwa mtaani na washabiki wazungumze zaidi kuhusu yeye.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...