Monday, July 18, 2011

Tattoo Recordz Kuwatoa Wasanii Wapya Wa Shindano la Jenga Nchi Yako

Mkurugenzi na mmiliki wa Tattoo Recordz akiwa ofisini kwake Masaki,DSM

Hapa ni nje ya Studio za Tattoo Recordz
Mkurugenzi wa Tattoo Recordz akiwa na meneja wa studio Abi MP

Hivi karibuni kuna mchakato wa kuchukua fomu ambao unaendelea kuhusu tamasha la kusaka vipaji linaliokwenda kwa jina la jenga nchi yako,likiwa limetayarishwa na Richard Manyota kama mratibu kutoka kampuni ya global publishers ambao ni watengenezaji wa magazeti ya ijumaa,uwazi,risasi,amani na champion,kwa kushirikiana na Police tanzania ambao ni wadhamini wakuu,lengo ni kupunguza lindi la uhalifu na kufanya Tanzania salama kupitia vipaji vijana walivyonavyo, na kama sehemu ya kuunga mkono harakati zote za kuleta amani na ajira kwa vijana Tattoo Recordz kupitia Mkurugenzi wake mkuu Bw Faraja kiobya Leguna ama Brother Tattoo kama anavyofahamika imetoa nafasi ya kurekodi kwa washindi watakaopatikana katika shindano hilo,brother Tattoo anashuka "sioni sababu ya kutowasaidia wasanii wachanga kutimiza ndoto zao kwani hata mimi mwanzo nilikuwa msanii na nafahamu ni adha gani wasanii wachanga wanazopata" ,shindano hilo litashirikisha wasanii ambao hawakuwahi kurekodi ama kuskika redioni tu, na fomu bado zinapatikana katika ofisi za global publishers bamaga na kwa maelezo zaidi soma magazeti pendwa yanayotengenezwa na global publishers niliyoyaorodhesha hapo juu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...