Wednesday, July 27, 2011

A.T na Baby J wamaliza tofauti zao rasmi

A.T katika pozi

Baby J.
Wasanii kioo kunako game ya Bongo wanaotokea visiwani Zanzibar, Baby J na A.T a.k.a Baba ntilie wamemaliza tofauti zao rasmi na kuamua kuachana na mambo ya mabifu wakidai hayana msingi kwani wanachoangalia sasa ni kusonga mbele na kutengeneza pesa, Credit nyingi zinaweza kumuendea mtu mzima G-Lover kwani ndiye aliyekuwa kiungo mchezeshaji kuhakikisha vijana hawa wanarudi upya katika maendeleo,kikao cha dharula kilichofanyika jumanne tarehe 26 mwezi huu wa saba katika sehemu ya vinywaji baridi na chakula ijulikanayo kama MAISHA PLUS ndicho kilichozaa matunda, kikiwahusisha pia watu kadhaa wa karibu na wasanii hao akiwemo mtu mzima SHARO MILIONEA, ALI MASTER, AUNTI kama wenyewe wanavyopenda kumuita ambaye ndiye mmiliki wa mgahawa huo wa Maisha plus, na swala likawa inakuwaje kuhusu nyimbo ambayo Baby J aliitoa akimponda mchizi na baby alikuwa na haya ya kushuka "yale yameshakwisha na A.T ni ndugu yangu hivyo ntaizuia ile nyimbo isipigwe na hata ule mpango wa video hauko tena na nimekubali yaliyopita yamepita" na A.T alikuwa na haya ya kusema "kwa mapatano haya basi tushasameheana na mimi namchukulia Baby J kama mdogo wangu hivyo yameisha na kuonyesha hatuna kinyongo tutagonga ngoma ya pamoja ila kibiashara zaidi", wakati huo huo inasemekana kuna watu hawakufurahishwa na kupatana kwa wasanii hawa kwani walikuwa wanachochea bifu hiyo kwa maslahi yao na wasanii hawa wanapenda watu wafahamu kuwa hawakulazimishwa kupatana ila wamepatana kwani ndicho kitu bora kwao kwa sasa kuliko malumbano yasiyokuwa na msingi, na mwisho kwa pamoja wakashuka "tunajua waliokuwa wanatugombanisha ni watu wetu wa karibu na walikuwa wanafanya hivyo kwa sababu zao na tunashukuru Mungu tumepatana na tumewajua wanafki", Credit zangu za dhati kabisa ziwaendee wasanii hawa kwa kuweka tofauti zao na kuanza maisha upya, lakini pili zimuendee mtu mzima G-lover, Sharo milionea, Ali Master na Aunti wa Maisha plus zanzibar kwa juhudi zao za kiubinadamu kuwaunganisha dada na kaka hawa waliopotea kwa malumbano, HONGERENI SANA BABY J na A.T kwa hatua mlizochukua.
From Tattoo Recordz Management.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...