Thursday, April 5, 2012

Tattoo Recordz introducing Triple Divaz

Logo namba moja ya Triple Divaz. 

Logo namba mbili ya Triple Divaz.

Hili ni kundi jipya la muziki la kinadada watatu akiwemo Cianna Jordan, Fantasia na hellens wakiwa chini ya Tattoo Recordz na Richard Manyota kama mratibu mkuu wa kundi hili, "kikubwa watu wanataka mabadiliko katika game n here we are" Mwanadada Fantasia akizungumza kwa niaba ya wenzie, Hellens akajazia "kikubwa watu wasitegemee kutuona tofauti ila wategemee kuona tofauti", Cianna Jordan kwa msisitizo "Hakuna kundi linalojumuisha wadada tupu Tanzania hivyo tunataka kulipa kipaumbele hilo na kuwakilisha mziki mzuri kama wafanyavyo Blue3 kutoka Uganda".

Wakinadada wana confidence ya kutosha juu ya wanachokifanya, nafasi ni yao na ni kweli tunahitaji kuona tofauti, wakizungumzia kuhusu Album ama nyimbo zao kuanza kusikika redio wanashuka "Album hapana kwa kweli bado sana, ila nyimbo soon enough tutaanza kuachia ila kikubwa kwa sasa tunaconcetrate katika project yetu tunayoifanya studio tofauti tofauti ikiwemo Akili Recordz, Tattoo Recordz, Kiumbe, Rama Recordz na nyinginezo nyingi chini ya watayarishaji Akili the brain, Pallah, Elter, Eagle master, Kitah, Jobiso, Ak Musicz na wengineo wengi".

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...