Friday, March 18, 2011

WAKWELI - NIMERUDI KUTOKA EUROPE KULETA MAPINDUZI BONGO

Wakweli in Holland
Jamaa akiwa anafahamika kama wakweli,ni Mtanzania anayeishi Europe kwa kipindi kirefu sana na  akiwa anafanya shughuli zake za kimuziki na masomo Barani humo,jamaa amekua akifanya ziara mbali mbali Barani Europe ikiwamo U.K ,Holland na Belgium, lakini akiwa ni mkazi wa muda mrefu nchini Holland kama mtanzania mwenye uraia wa nchi hiyo, lakini siku zote ndoto zake zilikuwa siku moja afanye muziki wa nyumbani kwao yaani Tanzania ambao amezaliwa,jamaa aliondoka nchini miaka mingi sana akiwa bwana mdogo,and now "WAKWELI IS BACK IN TOWN,BACK IN BONGO CITY".


Wakweli akiwa dukani kwake Msimbazi - Kariakoo. 


wakweli anazungumziaje ujio wake Bongo "kilichonileta Bongo ni kuleta mabadiliko,kwani naumia sana kuona wabongo wanahusle na kutumikia vitu vya wageni nchi za watu wakati Bongo inazidi didimia,mimi binafsi nimefanya mziki wa kidachi,kiingereza na kupata sifa kibao nchi za watu,sasa muda wangu umefika kuugeukia na muziki wa bongo",
Jamaa anaweza kiukweli na ana hasira haswa za kuleta mabadiliko,na kwa kuanzia harakati zake jamaa ameamua kuweka pia makazi bongo japo kwa muda,pili jamaa amefungua duka la pamba(nguo) za kisasa Mkunguni - Kariakoo ambapo kwa kufungua duka hilo vijana kadhaa wa kitanzania wamepata ajira,mwenyewe anasema "TIME WILL TELL".


Wakweli akiwa na mchizi wake wa ukweli kabisa msanii X- Dizo a.k.a D-boy

Wakweli akiwa na mkurugenzi wa Tattoo Recordz Gbroo a.k.a Tattoo dukani kwa Wakweli Kariakoo - Msimbazi.


Wakweli,x-Dizo na Mwajo


Wakweli akiwa na machizi wake wa kundi la "Kama mbele next level".


Wakweli ndo huyooooooooo from Holland to Bongo lets wait n we see what he dooooooes ma nicca.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...