Unapoizungumzia THT kwa sasa unaweza kumtaja Linah,Barnaba,Mataluma,Dito,Maunda,Amini,Mwasiti na wengineo wengi lakini list hiyo huenda isinoge (Shine) iwapo utalisahau jina la msanii mwenye makeke na vituko vingi vya kila aina toka panda hizo za Nyumba ya Vipaji,hapa tunamzungumzia msanii BUIBUI au BAIYA kama anavyopenda kujitambulisha kwa mashabiki wake,kwanini nimeuita moyo wa nyumba hiyo,kwa uelewa wangu msanii huyo ndiye msanii wa muda mrefu zaidi katika nyumba hiyo ya vipaji,akiwa na song yake ya NIMEKUSAMEHA alifanikiwa kuteka sana mashabiki kiasi cha kutishia uwepo wa wakongwe wa R n B kwa kipindi hicho lakini kwa sababu ambazo yeye binafsi anazifahamu alikaa kimya muda mrefu pasipo kusikika mpaka aliporudi tena.
BuiBui akiwa na msanii Jackson George wa BSS ndani ya studio za Tattoo Recordz.
Safari yake haikuishia katika NIMEKUSAMEHE, Mwaka uliopita jamaa alidondosha bonge la song lililokwenda kwa taito ya BORA NIIMBE ikiwa ni production ya Tattoo Recordz na kumuweka juu tena kiasi cha wadau kumzungumzia na kuamini amerudi tena,na mwaka huu jamaa anauanza mwaka kwa song inayoitwa SIJALI MABAYA ikiwa pia ni production ya Tattoo Recordz chini ya producer Baba Byson a.k.a JOBISO, ni ngoma yenye ufundi wa kutosha kuanzia midundo,sauti mpaka mashairi, imeshafanyiwa video na audio yake pia imeshasambazwa vituo vya redio hivyo soon itaanza kusikika ,na pia inapatikana katika playlist ya blog hii ya Tattoo Recordz.
No comments:
Post a Comment