About Tattoo

Tattoo Recordz ni moja kati ya studio zenye mafanikio ya kutosha kunako game ya muziki wa Tanzania,katika muda mchache tu iliyoanzishwa (mwezi mmoja ) iliweza kutimiza malengo yake kwa asilimia kubwa na kuwa ni moja kati ya studio zinazosumbua kunako muziki,ilianzishwa 13-03-2010 kama njia mojawapo ya kuwasaidia vijana kutimiza malengo yao ya sanaa na muziki kiujumla, na mpaka sasa imeshafanya kazi na wasanii tofauti  akiwamo A.T,Dorika, Maunda Zorro,Dokii, Pingu, Barnaba, Tunda Man, Beka, Hardmard, Emax, Mataluma, Steve wa R n B, Mansulii, Nash MC, QJ,Mrisho Mpoto,  Sapeleme, BuiBui, Baby J, THT, Nuruelly, Mjomba band,Joan,Banana Zorro,Richard Marions na wengineo wengi katika tasnia hii ya muziki.

MATALUMA
Ngoma ambayo inamuunganisha Mataluma na Tattoo Recordz inakwenda kwa jina la SABABU YAKO,Jamaa anaweza kiukweli na mmoja kati ya wasanii wachache wasiofanana na mtu yoyote kwa mitindo ,aina ya nyimbo mpaka kuongea,BIG UP MATALUMA,kaza buti.


MAUNDA ZORO
Kama utaniuliza kwa Tanzania nani ni best female vocalist,basi Maunda Zoro nisingesita kumtaja,huwa ananikosha sana kwa sauti yake nzuri anapoimba kwa ustadi mkubwa,Huwa natamani kumuona tena na tena,na ngoma inayomkutanisha na Tattoo Recordz inakwenda kwa jina la NALIA,ni bonge moja la ngoma ya zouk na Maunda amelia si mchezo,kila la kheri.


MJOMBA BAND
Kwa mara ya kwanza ukimsikia lazima upatwe na maswali mengi yanayokosa majibu,lakini kwa mara ya kwanza pia unapowasikia kama Band unaweza usiamini kwa jinsi mirindimo ya sauti na ala zinavyochanganywa na kupata ladha moja ya kiafrika,wanaitwa mjomba band ni moja kati ya makundi mengi Tattoo Recordz iliyowahi kufanya nayo kazi lakini kundi hili likichukua nafasi muhimu na ya kiheshima zeidi kwa jinsi inavyotambua matatizo ya kijamii,kiongozi wake anaitwa Mrisho Mpoto na nyimbo inayoiunganisha Band hii na Tattoo Recordz inaitwa DIRA YA TAIFA,pongezi kwa mjomba na Mjomba Band.

BARNABAS
Wengi wanamfahamu kama Barnaba,jina lake kamili anaitwa Barnabas Elias kijana anayetokea nyumba ya vipaji (THT),akiwa  kama muimbaji na mwalimu msaidizi, nyimbo inayomkutanisha na Tattoo Recordz inaitwa SIDILI NA WEWE akiwa na msanii kutoka visiwani Zanzibar anayekwenda kwa jina la Baby J,kazi nzuri na bado tunasafari ndefu ya kuzidi kumuona Barnabas akitawala na kuiongoza vyema THT na muziki kiujumla.

STEVE R n B
Anaitwa Steve wa R n B na nyimbo inayomuunganisha na Tattoo inakwenda kwa jina la ONLY YOU,jamaa akiwa ameandika vya kutosha na kugongeza midundo yenye ujazo wa kutosha.

NASH DIZAINA kutoka THT
Kwa mtazamo wa karibu na rahisi unaweza usiuone umuhimu wa huyu jamaa,lakini unapomuuliza msanii yoyote kutoka THT unaweza pata picha kamili ni muhimu kiasi gani,ana sauti,mtindo,na pia ni mwalimu msaidizi THT,Big up Nash Dizaina.


BEKA
(wa katikati)
Kwa mara ya kwanza namuona Beka sikuamini kile anachokiimba na umri wake,ni mmoja kati ya wasanii wenye vipaji vya hali ya juu sana,na ngoma inayomkutanisha na Tattoo Recordz inaitwa NATUMAINI REMIX,ikiwa na kila aina ya ufundi,kwa akili ya haraka si rahisi mtu kufanya alichofanya Beka na hapo ndo unapoonekana utofauti kati ya Beka na wasanii wengine,ONE LOVE BEKA.


Kazi zote hizi na wasanii wote hawa wanaunganishwa kupitia Tattoo recordz iliyoko mwananyamala,komakoma,karibu na masai club/Meridian Hotel,na utengenezaji mziki ukisimamiwa na watayarishaji wanne wenye ujuzi,uzoefu na vipaji tofauti(AK47,JOBISO,PALLAH,ELTER). 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...