Saturday, March 19, 2011

ZAVARA - Mwanaharakati wa HipHop anayeitunza na kuijali kama mwanae wa kumzaa.

Jina hili si geni masikioni mwa watu wengi wanaofatilia muziki wa Hiphop ,ZAVARA ndo jina , Hiphop ndo muziki unaompa heshima kila siku na kila sehemu,wengi watakuwa wanakumbuka ile michano ya pale BRITISH COUNSEL kila jumapili ama jumamosi kwani iliwapa ramani wasanii kibao wa Hiphop ,Nash MC akiwa shahidi tosha wa harakati za mtu mzima Zavara.


 Zavara akiwa katika mkao wa uhamasishaji wa Hiphop ndani ya Tattoo Recordz.

 Zavara katikati akiwa na producer AK47(kushoto) na meneja wa Tattoo Recordz "ABI"


 Zavara akiwa na mwanaharakati mwingine na msanii wa siku nyingi Prof Jay


Zavara akiwa na mkurugenzi wa Tattoo Recordz "Brother Tattoo".


Mwanaharakati Zavara anasema "Unajua Hiphop ni Heshima na kama umekosa heshima umekosa Hiphop,hivyo Hiphop ina misingi na njia zake na ndiyo inayonifanya niwe na moyo wa kuipigania na kuipa haki kwa kila anayeigusa kwa ubaya",


Zavara yuko katika mpango maalum wa kuinua Hiphop akishirikiana na Tattoo Recordz chini ya Brother Tattoo na clue nzima ya maproducer watatu kutoka Tattoo wanaofanya midundo ya Hiphop yaani Pallah ,AK47 na Elter. Hivyo wadau na wanaharakati wa Hiphop inawahusu hii kwa asilimia zote,kuwa tayari utajulishwa siku hadi siku,
SHUKRANI ZIWAENDEE KAKA ZAVARA NA TATTOO RECORDZ.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...