Wednesday, March 30, 2011

Bata Hawezi kuwa kuku kamwe hata awekwe spice za kutosha na mazagazaga kibao.

                                                            Bata ni Bata tu.
                                                           Na kuku ni kuku tu.
Bata Hawezi kuwa hivi hata umuweke spice na mazagazaga kibao kwani kuku ni kuku


Kila Mwenye Amani na iwe nae,na ole wake mnafki kwani ataumbuka na ukweli utabaki kuwa ukweli, Sizungumzi kwasababu napenda kuzungumza ila nazungumza sababu nina mapenzi na ya dhati na kile ninachokifanya kila siku.
Chaguo langu lilikuwa muziki kabla hata sijamaliza shule ya msingi, na imani ya muziki ndio shuka pekee nililojifunika miaka mingi iliyopita mpaka leo hii,toka wakati naimba mpaka leo hii nikiwa Mkurugenzi wa Recordz label inayowafanya watu wasilale ya Tattoo Recordz,si kwa kuwa inaendeshwa kibabe, La hasha, ni kwa upendo,uvumilivu na ushirikiano wa hali ya juu.
Ni mengi yanayonifanya niandike Kurasa hii lakini ni swala haswa la watu wachache kuumiliki muziki na si jamii, INAUMA SANA sababu tunaujua na kuufahamu kuliko wanavyoufahamu wao,hebu ngoja kwanza "We Shabani wakati ule unajiita Tozi mtoto kabla hujapewa kitengo cha ufagiaji sisi si tulikuwa tumeshaanza kuchana(kuimba hiphop)?",anyway kila lenye mwanzo halikosi mwisho, na kila amuombeaye mwenzio mabaya iko siku yake.


Watu hatulali sababu kuna panya anasumbua usiku kwa kelele zake chini ya kitanda na kabati ,kwani yeye ni panya wa aina gani hata paka mkubwa aliyepewa dhamana ya kulinda nyumba akashindwa kumuwinda.
Ishaalah na ugumu wote ninaoupata,majungu yote yanayopigwa hayanisumbui kichwa kwani mkeo hata akikutusi hakutoi uhai ni hulka tu inayomfanya apende kuonekana nae yumo katika kundi la mashoga zake,Na kama nilivyoianza safari kwa ugumu ndivyo mtakavyoimaliza nyie kwani hata wale Bata wenu mnaowafuga na kutulingishia mtaani kuwa ni bora watawageuka na kuujua ukweli ambao mmejaribu kuuficha kwa muda ,ila ikumbukwe tu Bata hawezi kuwa kuku hata umuweke kiuongo cha aina gani.


Amani kwa wanangu wote wa ukweli,Amani kwa Producers wote wa ukweli,Amani kwa Presenters wote wa ukweli, Muziki ni vita hivyo tetea Taifa lako,HipHop for Life.
PAMOKO SANA,


Managing Director,
Tattoo Recordz.

2 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...