Kalama Masoud a.k.a Kalapina katika pozi.
Msanii Ibrah Rush ambaye ameshiriki katika Kuidisi Serikali akiwa na Kalapina.
Msanii nguli na mwanaharakati wa hiphop toka pande za Block 41 na kiongozi wa kundi la muda mrefu katika game la KIKOSI CHA MIZINGA Kalama Masoud a.k.a Kalapina, anatarajiwa kufanya makamuzi ya kutosha katika uzinduzi wa album yake mpya ya MAISHA YANGU NYIMBO TOSHA ndani ya NEW MAISHA CLUB pande za Obey Dar es saalam, Uzinduzi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 27/03/2011 (Ni siku chache tu zijazo).
Nini haswa ambacho kimewavutia wadau katika uzinduzi huu,Msanii QJ anasema "Mimi ntavutiwa sana na show nzima sababu mzigo wa kalapina stejini naujua lakini zaidi ni ile ngoma inayoitwa SERIKALI,Pina amekamua sana na kuongea ukweli mtupu akishirikiana na mchizi Ibrah Rush,sijui stejini siku hiyo itakuwaje?",Mdau mwingine ambaye ni director mzuri wa video toka pande za kiumbe ABYKAZ akasema "Jombaa Namuheshimu kalapina,ile michano yake usipime na ile ngoma aliyoidisi serikali jombaa kakamuaaaaaaa".
SERIKALI ni ngoma ambayo Kalapina amefanya na msanii Ibrah Rush wakiidisi serikali vilivyo na ikiwa imefanyika ndani ya studio za Tattoo Recordz Komakoma - Mwananyamala,katika uzinduzi huo ngoma hii inategemewa kutambulishwa na kuwa kivutio kwa jinsi Msanii kalapina alivyoonyesha uzalendo kwa Watanzania wenzie kwa kuyatambua matatizo yao na kukemea hali zote zinazofanya watu wawe na maisha duni.
Haya wadau kalapina na serikali kunani?,Binafsi siwezi kukosa uzinduzi huo kumshuhudia mwanahiphop wa kweli akitetea watanzania wenzie dhidi ya serikali,ngoma inapatikana katika Tattoo Recordz playlist humu katika blog.

No comments:
Post a Comment