Thursday, April 28, 2011

Yajue Majengo Kumi Ya Thamani Zaidi Duniani Kwa Sasa.

1.ANTILLA, Jengo hili linapatikana Mumbai nchini India ndilo linaloshika namba moja likiwa na thamani ya Dolla Billioni moja (1bil USD), Jengo hili linamilikiwa na tajiri namba nne kwa pesa duniani bwana Mukesh Ambani ambaye ni raia wa India na jengo lina urefu wa futi 570 na uwezo wa kuchukua wafanyakazi 600 ndani yake.

2.VILLA LEOPOLDA linalopatikana Cote d'Azur nchini Ufaransa lina thamani ya Dolla Millioni mia tano na ishirini na tano (525Mil USD),jengo hili lilijengwa mwaka 1902 na mfalme Leopold wa pili wa Ubeljiji na kumekuwa na tetesi kuwa jengo hili ni makazi ya tajiri na mmiliki wa microsoft bwana Bill Gates japo ukweli ni kuwa jengo hili linamilikiwa na mfanyabiashara wa benki wa kifaransa bwana Edmond Safira ambaye mkewe ndiye anayeishi hapo kwa sasa,hili ndilo linaloshika namba mbili (2) kwa thamani duniani.

3.ONE HYDE PARK linalopatikana Penthouse jijini London Uingereza ndilo linaloshika namba tatu kwa thamani duniani likiwa na thamani ya Dolla Millioni mia mbili (200mil USD),jengo hili linalindwa na wanajeshi wakufunzi wa hali ya juu wa kiingereza ambao wanafanya kazi za kijeshi kwa usiri wa hali ya juu yaani (SAS),pia limejengwa na madirisha yanayozuia risasi kupenya, pia limewekwa vitambua jicho (Iris Scanners),pia kuna chumba taarifa cha kutoa  kelele (panic room) na handaki la siri lililochimbwa mpaka karibu na hotel ya Mandalin inayopatikana umbali kidogo kutoka katika jengo hilo la kuvutia.

4.FAIRFIELD POND likiwa linapatikana The Hamptons nchini Marekani ndilo haswa jengo kubwa kwa makazi ya kawaida ya kuishi likiwa na heka 63 vyumba vya kulala 29 vinavyotazamana na bahari,sehemu ya kurushia vitufe, ni makazi ya bilionea mwenye aibu ya kujitangaza ama kujulikana Ira Rennert, jengo lina viwanja vitano vya michezo,jengo hili lina thamani ya Dolla zipatazo millioni mia na sabini (170mil USD).

5.HEARST MANSION likiwa Bevery Hills nchini marekani ndilo jengo linaloshika namba tano kwa thamani likifikia Dolla milioni mia sitini na tano (165mil USD), hekalu hili linajulikana kama makazi ya zamani ya mwandishi mkubwa na bora bwana William Randolph japo lilipata umaarufu haswa pale lilipofanyiwa uchukuaji wa picha wa filamu ya GODFATHER na haiwezi kusahaulika kuwa rais wa zamani wa marekani aliyeuawa John .F. Kennedy alikaa hapa katika kipindi cha fungate la harusi yake (Honeymoon),nyumba hii inapakana na makazi ya watu maarufu akiwemo David Beckham na mkewe, Tom Cruise na Katie Holmes.

6.FRANCHUK VILLA likiwa linapatikana Kensington thamani yake inafikia Dolla mia sitini na moja (161mil USD) mwanzo lilijulikana kama The Victorian Villa na lilikuwa ni shule ya maandalizi kwa watoto wa kike mpaka mwaka 1997 liliponunuliwa na kuongezwa vitu vya thamani mwaka 2006, na baadae lilikuja kununuliwa na Elena Franchuk ambaye ni mtoa misaada mkubwa wa masuala ya ukimwi mwenye asili ya Ukraine baada ya jengo hilo kufanyiwa ukarabati na marekebisho yaliyofikia kiasi cha Dolla milioni kumi (10mil USD) na kulipa jina la Franchuk Villa kwa heshima ya familia yake.

7.THE PINNACLE likiwa linapatikana Montana linafikia thamani ya Dolla milioni mia hamsini na moja (151mil USD) linamilikiwa na matajiri Time na Edna Blixseth wanaomiliki Billionaires-only golf and sky resort "yellowstone club" inayopatikana Montana, jengo hili lina vivutio tofauti ikiwamo joto linalopatikana katika kila inchi moja ya sakafu,sehemu ya moto (fire place) katika kila bafu na vyumba kumi tu vya kulala.

8.THE MANOR ikiwa Los Angeles Marekani ina thamani ya Dolla milioni mia na hamsini (150mil USD) ni makazi ya Aaron Spelling na mkewe Cindy ina jumla ya vyumba 123,majiko matatu, bustani binafsi ya matunda, sehemu ya mchezo wa kurushia tufe(bowling alley), viwanja vya michezo, sehemu ya kufungia zawadi na sehemu ya chini ya jengo ni kwa ajili ya makabati tu.

9.UPDOWN COURT inayokadiriwa kuwa na thamani ya Dolla milioni mia na thelasini na tisa (139mil USD), uzuri wa jengo hili unapolitazama kwa juu na mwaka 2008 ndilo jengo lililoshika nafasi ya tatu kwa thamani zaidi duniani likiwa na thamani ya dolla milioni mia na kumi tu (110mil USD) ikiwa na maana kuwa thamani ya jengo hili imepanda kwa kasi sana ukiachia mbali matatizo ya kiuchumi yaliyoikabili dunia, jengo hili linapatikana Windlesham,Surrey.

10.DRACULA'S CASTLE nchini Romania lina thamani ya Dolla milioni mia thelasini na tano (135mil USD) jengo hili lilijengwa katika karne ya kumi na nne na kwa sasa linatumika kama makumbusho ya taifa,lina vyumba 57 ikijumuisha vyumba vya kulala 17 vilivyopambwa na thamani ya vito vya karne zilizopita na vitu vya kihistoria na inakadiliwa kuwa makumusho haya hutembelewa na watalii wafikao milioni mia nne na hamsini (450 mil tourists) kila mwaka.

Hayo ndiyo majengo kumi yenye thamani zaidi duniani kwa sasa baadhi yakiwa ni makazi ya watu,makumbusho,sehemu za biashara ,na majengo ya kihistoria na majengo ya serikali.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...