Monday, April 25, 2011

Pata Kuzifahamu Gari Kumi Za Gharama Na Thamani Zaidi Duniani Kwa Sasa.

 Hii Inaitwa Buggati Veyron ikiwa inauzwa Dolla millioni moja na laki saba (1,700,000) ikiwa na spidi kubwa ya 267mph+ na uwezo wa kwenda 60mph kwa sekunde 2.5, hivyo kuifanya kuwa gari yenye spidi kubwa zaidi ikishika namba moja duniani na pia kuwa gari ya gharama kubwa zaidi kwa matumizi ya kawaida.
 Inaitwa Lamborghini Reventon inauzwa Dolla Millioni moja na laki sita (1,600,000) ikiwa na uwezo wa kwenda 60mph kwa sekunde 3.3 na imebarikiwa spidi ya 211mph+ hivyo kuifanya gari ya pili kwa gharama duniani.
 MacLaren F1 ,ikiwa na uwezo wa kutembea 60mph kwa sekunde 3.2 na spidi kubwa ya 240mph+, inapatikana kwa Dolla Laki tisa na sabini (970,000) hivyo kuifanya kuwa gari ya tatu kwa spidi zaidi miongoni mwa magari ya gharama kwa muda mrefu kidogo.
 Ferrari Enzo Spidi ya 60mph kwa sekunde 3.4 na spidi ya kawaida ya 217mph+, huku ikishika namba nne na kuwa gari ya gharama kwa kuuzwa kiasi cha dolla laki sita na sabini (670,000). 
 Namba tano ni Pagani Zonda C12F ikiuzwa Dolla Laki sita na sitini na saba mia tatu na ishirini na moja (667,321) na ikiwa na spidi ya 215mph+ na uwezo wa kwenda 60mph kwa sekunde 3.5,imetengenezwa nchini Italy.
 Hii inaitwa SSC Ultimate Aero ikiuzwa Dolla laki sita hamsini na nne mia nne (654,400),ikitembea na spidi kubwa ya 257mph+ na uwezo wa kwenda 60mph kwa sekunde 2.7 hivyo kuipa ushindi wa pili wa kuwa gari yenye spidi zaidi kwa kipindi hiki kwa matumizi ya kawaida.
 
 Saleen S7 Twin Turbo ndio jina ikiwa na thamani ya Dolla Laki tano na hamsini na tano elfu (555,000) na uwezo wa kutembea 60mph kwa sekunde 3.2 na spidi ya 248mph+ na kuifanya kuwa gari ya tatu kwa spidi kubwa zaidi.
 Koenigsegg CCX ikiwa inauzwa Dolla Laki tano arobaini na tano na mia tano sitini na nane (545,568) ikiwa ya nne kwa spidi duniani ikiwa na spidi ya 245mph+.
 Mercedes Benz SLR MacLaren Roadster ikiwa na thamani ya Dolla Laki nne na tisini na tano (495,000),ikipewa uwezo wa kwenda 60mph kwa sekunde 3.8 na spidi ya 206mph+.
Gari ya kumi inaitwa Porsche Carrera GT ikiwa na thamani ya Dolla Laki nne na arobaini (440,000) ikiwa na uwezo wa kutembea 60mph kwa sekunde 3.9 na spidi kubwa ya 205mph+.


Haya Takwimu zinaonyesha hivyo na kila mtu ana malengo yake hivyo kama ulikuwa na mpango wa kumiliki gari ya thamani why dont you try Buggati?,na kama unadhani ndoto zako zinaishia kwenye Corolla basi baki na Corolla.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...